Makampuni 25 kujadili fursa za biashara nchini DRC

Tanzania inatarajia kutuma ujumbe wa wafanyabiashara zaidi ya 100 kwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kushiriki Kongamano la biashara lijulikanalo kama Tanzania DR Congo Trade Forum litakalofanyika Septemba 22 katika jiji la Lubumbashi.

Kongamano hilo limeandaliwa na asasi ya 361 Degrees na kuratibiwa na taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ikishirikiana na taasisi za umma kama TCCIA, Tantrade, pamoja na Shirikisho la Wafanyabiashara wa Congo (FEC), likiwa na lengo la kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili kama anavyoeleza mwakilishi wa TPSF Bw. Louis Accaro.

Kongamano hilo limetajwa kuwa ni fursa muhimu kwa makampuni ya Kitanzania na kwamba Kongo imekuwa ni soko zuri la bidhaa za kilimo ikiwemo vyakula pamoja na samaki wakavu kwani hali hiyo imechangiwa na kukosekana kwa amani ambako kumewafanya wananchi wa nchi hiyo kukosa muda wa kuandaa mazao yao.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items