Dodoma. Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amekabidhiwa kitambulisho chake cha Taifa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba leo mjini Dodoma ambacho kinaonesha picha yake, saini yake pamoja na saini ya mtoa kitambulisho.
Hatua hiyo ya Spika Ndugai ya kupokea kitambulisho hicho ni mkakati wa taifa ambao NIDA imekusudia kukamilisha usajili wa vitambulisho vya taifa nchi nzima kwa wananchi, wageni na wakimbizi ifikapo Desemba mwaka huu pamoja na kutoa namba ya utambulisho ambayo itawezesha makundi yote kupata huduma mbalimbali.
Ili kufikia malengo ya usajili wa ya kusajili Watanzania milioni 24, NIDA imekusudia kutumia taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) milioni 22.7 ambazo watachakatwa na kutoa namba ya utambulisho (NIN) kabla ya kuzalisha kitambulisho cha taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumkabidhi Spika kitambulisho hicho, Waziri Mwigulu amesema kuwa mfumo wa utambuzi na usajili wa watu utasaidia kuwaunganisha wananchi na mifumo mingine ya huduma ikiwamo mifuko ya hifadhi za jamii, benki, Bodi ya mikopo ya elimu ya juu, RITA na TCRA pamoja na taasisi nyingine zinazotoa huduma.