Sumbawanga. Mwalimu wa Shule ya Sekondari Usevya, wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi, Makonda Ng’oka (34) anadaiwa kupigwa hadi kung’olewa meno matano na wanafunzi wake.
Kipigo dhidi yake kinatakiwa kufanywa na baadhi ya wanafunzi wake wa kidato cha sita kwa madai ya kuwadhalilisha wavulana.
Ng’oka amedai alivamiwa akiwa nyumbani na kumshambulia yeye na familia yake kwa kutumia silaha za jadi.
Mwalimu wa shule hiyo, Gabriel Kambona ambaye naye amedai kupigwa amesema hayuko tayari kufundisha shule hiyo kwa kuwa kitendo hicho kimemfedhehesha.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Katavi, Gregori Mshota amekiri kufahamu mkasa huo.
“CWT imewasiliana na uongozi wa Halmashauri ya Mpimbwe na Wilaya ya Mlele ili kuhakikisha mwalimu huyo anakuwa salama. Jambo hili halihitaji mjadala zaidi kinachotakiwa kupangiwa kituo kingine cha kazi ili kunusuru maisha yake,”amesema.