Wiki ya nenda kwa usalama kuanza Septemba 26

Dar es Salaam.Kikosi cha Usalama Barabani kimetangaza wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo itaadhimishwa kitaifa mkoani Geita kuanzia Septemba 26 hadi Oktoba Mosi mwaka huu na kuwataka wenye magari na pikipiki kupeleka kwenye vituo vya trafiki kwa ajili ya ukaguzi.

Akizungumza leo, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema vyombo vya moto vitatakiwa kukaguliwa na kupewa stika maalum.

Amesema gharama ya stika hizo kwa magari ya biashara zitauzwa kwa Sh5, 000, magari madogo binafsi Sh3000 na pikipiki na bajaji Sh1, 000.

Amesema stika hizo zitasaidia kuyabaini magari mabovu ambayo hayana sifa za kutembea na kuyaondoa kabisa barabarani.

Mpinga amesema mbali na ukaguzi huo kufanyika katika vituo vya trafiki, kila mkoa utaainisha maeneo mengine kwa ajili ya ukaguzi wa vyombo hivyo vya moto.

Mpinga amesema ubovu wa vyombo vya moto ni miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha ajali za barabarani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items