Mwanamke anyimwa kazi kwa kuwa na rasta

Mwanamke anyimwa kazi kwa kuwa na rasta Marekani

Kampuni moja iliokataa kumuajiri mwanamke mweusi kwa sababu alikataa kuzikata nywele zake za rasta.Mahakama ya rufaa nchini Marekani imetupilia mbali kesi dhidi ya ka

Chastity Jones alituma ombi la kazi katika kampuni moja ya kukabiliana na majanga ana akaajiriwa.
Lakini ilikuwa chini ya sharti kwamba ni lazima akatwe nywele zake.Meneja anayesimamia maswala ya wafanyikazi inadaiwa alimwambia kwamba nywele zake hazimbatani na sera za kampuni kwa sababu ''hukera'.

Tume ya fursa sawa za ajira nchini humo EEOC inaamini kwamba hatua ya kampuni hiyo ilienda kinyume sheria ya haki za raia ya mwaka 1964.

Tume hiyo ilihoji kwamba kupiga marufuku rasta kazini ni ubaguzi wa rangi,kwa sababu rasta zinahusishwa sana na watu wenye asili za Kiafrika.