Serengeti Boys Watua Congo Brazaville Leo

  Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda walikopiga kambi kabla ya kuwavaa vijana wenzao wa Congo Brazaville Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Massamba Sebat, Brazzaville.  Timu hiyo imefikia Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini humo. Kikosi hicho kimetua salama salmin kujindaa kuifumua Congo Jumapili.

Kutoa kushoto, Kibwana Shomari, Yohana Mkomola na Rashid Ada wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda.

 Wakiingia Hotelini.

  Serengeti Boys wakiingia Hotelini.

Makocha wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Muharami Mohammed Sultan maarufu kama Shilton (kushoto) anayewanoa makipa, Kocha Mkuu Bakari Nyundo Shime au Mchawi Mweusi na Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini Brazzaville, Congo.