Thabit Abdul aahidi kuipeleka taarab kanisani

Mkali wa muziki wa taarabu Thabit Abdul amesema ana mpango wa kusapoti kukua kwa muziki wa Injili kwa kufanya gospel yenye mahadhi ya taarab akiita "GOSPEL-TAARAB".

Akipiga story na eNewz Thabit Abdul amesema anaamini mashabiki wa muziki wa Injili wataupenda muziki huo, kwani ujumbe utabaki uleule wa maneno ya Mungu lakini atakachobadilisha ni midundo tu na kuifanya iwe ya taarab.

"Watu wengi wa Gospel waliwahi kunitafuta tufanye muziki wa Injili wa taarabu" alisema Thabit, na kuongeza kuwa "Tutatumia muziki huo kutoa neno la Mungu, lakini inapofika mwisho wa nyimbo basi lazima watu wacheze so hapo tutawasebenesha, na pia vidole juu lazima viwepo".