Alama ya Halaal katika vyakula,matunda na Vinywaji inatarajia kuanza kutumika

Baraza kuu la waislam nchini Tanzania limesema nembo ya Alama ya Halaal katika vyakula,matunda na Vinywaji inatarajia kuanza kutumika mwezi januari mwakani baada ya kukamilika taratibu za kuwaelimisha wazalishaji wa vyakula,matunda na vinywaji lakini pia baada ya wataalam kutoka nchini malaysia kukamilisha kutoa mafunzo hapa nchini.

Katibu Mkuu wa baraza kuu la waislam Tanzania Sheikh Suleiman Lolila akizungumza na waandshi wa habari jijini dsm amesema wataalam kutoka ofisi ya waziri wa dini wa Malaysia walikuwapo hapa nchini kutoa mafunzo,ambapo maabara maalum imetayarishwa ya kuangalia bidhaa,vyakula na vinywaji ambapo pia tanzania itapata nembo ya Jacklin ya nchini Malaysia na kuwezesha bidhaa zetu kuuzwa katika nchi la Ulaya,japan,amerika na Bara la arabuni.

Wataalam wa Halaal wawakilishi wa waziri wa Mambo ya Dini wa Malaysia wamesema mpango huo utasaidia kupanua soko la bidhaa za vyakula na Vinywaji lakini pia utasadia kuonyesha wazi mchanganyiko wa vyakula ili wale wasiohitaji kula vyakula aina fulani waviepuke.