Davido Awapigia Magoti Wanigeria

 STAA wa muziki wa Nigeria, Davido (pichani juu) amewaomba Wanigeria kumpa muda rais wa nchi yao, Muhammadu Buhari kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili nchi hiyo, ambapo amewaomba wampe muda atairejesha nchi sehemu nzuri.


Muhammadu Buhari.

Davido, baba wa mtoto mmoja, amesema anaamini Buhari ni kiongozi mzuri lakini anahitaji muda kuiweka nchi sehemu nzuri kiuchumi. Kwa sasa nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ikidaiwa kuwa uchumi wake umeshuka na kusababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo pia.