Mabaharia 26 waliotekwa Somalia miaka 5 iliopita waokolewa

Maafisa wa kimataifa wanoahusika katika majadiliano ya kufanikisha kuwachiwa kwa mateka wanasema mabaharia 26 waliokuwa wamezuiwa na maharamia wa Kisomali kwa takribana miaka mitano wamechiwa huru.

Wanaaminika kuwa miongoni mwa mamia ya mwisho ya mateka waliokamatwana maharamia wa Kisomali tangu katikati ya miaka ya 2000.

Uharamia kutoka pwani ya Somalia umepungua kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.
Mnamo Machi 26 mwaka 2012 Maharamia wa Kisomali waliivamia meli FV Naham 3 ilipokuwa inaeleka Usheli sheli.

Waliiteka meli hiyo na mabahari waliokuwemo ndani.
Takrian mwaka mmoja baadaye, meli hiyo ilizama. Mateka walifikishwa pwani ya Somalia na kuwekwa katika hali mbaya.

Tofauti na visa vingine, hapakuwa na kitita cha pesa kilichowasilishwa kutoka kampuni iliyomiliki meli hiyo.

Lakini majadiliano ya miaka kadhaa ya kudni dogo la watu wanaojitahidi kuwaokoa mabaharia waliosahauliwa hatimaye yamefua dafu.