Majambazi wanne wameuwawa na Polisi katika kijiji cha Mtambani Mkuranga mkoani Pwani

Majambazi wanne wameuwawa na Polisi katika kijiji cha Mtambani mkuranga mkoani Pwani wakati wakirushiana risasi na Polisi wakati polisi walipovamia nyumba mmoja ya watuhumiwa hao ambapo pia polisi mmoja amejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya Muhimbili.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi wa Temeke Giles Muroto akizungumza na waandshi wa habari amesema Mapambano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 20 yamesababisha pia kupatikana kwa bunduki moja ,risasi za bastora,ambapo majambazi zaidi ya watano walitoroka katika mpambano huo.

Aidha kamanda Mroto amesema Operesheni ya kuwasaka majambazi kwa kushirikikiana na kikosi maalum cha mkoa wa pwani kinaendelea na kutoa wito kwa wananchi kutoa Ushirikiano lakini pia kuwaonya wale wanaoshirikiana nao na kuwahifadhi majumbani.