Makachero Uwanja wa ndege Dar, wamtia mbaroni mwanamke akiwa na dawa za kulevya

Makachero katika Uwanja wa ndege wamemtia Mbaroni mwanamke Raia wa Brazil akiwa na Dawa za Kulevya
screen-shot-2016-10-20-at-2-59-54-pm

Makachero katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julias Mwalimu nyerere wamemtia Mbaroni mwanamke Lilian Jesus Fortes mwenye umri wa miaka 32 Raia wa Brazil ambaye baada ya kupekuliwa alikutwa na Dawa za Kulevya aina ya Cocaine kilo 2 na Robo ambazo aliziweka katika begi.

Kamanda wa Polisi kikosi cha Uwanja wa Ndege Martin Otieno akizungumza na Chanel amesema Mwanamke huyo alikuwa ameshuka katika ndege ya Etihad akitokea Katika mji wa Sao Paul nchini Brazil na baadae kupitia Abu dhabi ambapo alifika katika uwanja wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya kuunganisha safari na shirika la ndege la Ethiopia kuelekea nchini Malawi.

Amesema Mtuhumiwa huyo alikuwa amezifunga na kuhifadhi katika pakiti za Aluminium ambapo na kushonea Vizuri katika begi huku pembeni akiweka vitabu ili zisibainike katika mashine maalum za Ukaguzi.

Kamanda Otieno ameeendelea kuwaonya watu wote wanaotumia uwanja huo kupitisha dawa za kulevya au nyara zozote za Serikali kuwa wamejipanga na wale watakaojaribu watakumbana na Mkono wa sheria.