Rais wa Uganda arudi shambani

 Rais wa Uganda Yoweri Museveni amerudi shambani kwake ambapo atakuwa kwa kipindi cha juma moja akikuza kilimo mbali na kusimamia miradi ya serikali katika wilaya ya Lowero.

 Msafara wa rais sasa utakuwa wa baiskeli kwa muda ambayo atatumia kuteka maji ili kunyunyizia mimea.

Kulingana na msemaji wa serikali,Museveni tayari amekuwa akiwaonyesha wakaazi jinsi ya kupanda migomba na kahawa kwa kutumia chupa za plastiki ili kunyunyizia maji.