Sababu kuu 2 za Samsung kusitisha utengenezaji wa Galaxy Note 7

Mtandao wa Reuters umeripoti kuwa Samsung wameamua kusitisha utengezaji wa simu aina ya Galaxy Note 7 ili kuzifanyia ukaguzi zaidi.
spiralbinder-2016-2111-044
Leo October 10, 2016 nimezipata sababu kubwa 2 zilizopelekea Samsung kusitisha utengenezaji wa mzigo mwingine na kuziondoa sokoni kwa muda simu hizo ikiwa ni baada ya kampuni kubwa mbili za nchini Marekani kukataa kuendelea kuuza simu za Galaxy Note 7. Sababu hizo ni pamoja na..
  1. Kukagua kwa undani matatizo ya Betri za simu hizo ili kubaini ubovu wake.
  2. Kuimarisha utengezaji wa simu hizo ili kuhakikisha ubora na usalama wake
Kampuni ya Samsung leo Jumatatu October 10, 2010 imeshatangaza kuzuia usafirishaji wa simu hizo katika maeneo tofauti duniani ili kuzifanyia ukaguzi wa kina.
Ikumbukwe kwamba Kampuni hiyo ya Korea Kusini mwezi September ilizirudisha simu hizo na kuwahakikishia wateja wake kwamba simu zilizorekebishwa ziko salama, pamoja na taarifa hiyo ya Samsung bado kumekuwa na ripoti nyingine tofauti za simu zilizorekebishwa kuendelea kutoa moshi au kulipuka.
Mpya zaidi Nzee zaidi