VIDEO: Sababu za wanafunzi Tegeta Sekondari kugoma

shule ya sekondari Tegeta iliyopo jijini Dar es salaam wanafunzi wake wamegoma na kuandamana kuelekea kwa mkuu wa shule kwa madai kuwa walimu hawangii madarasani kufundisha aidha miiundombinu ya shule hiyo kutokuwa ya kuridhisha yakiwemo madarasa na vyoo.

Baadhi ya wanafunzi  wamesema walimu wamekuwa hawaingii madarasa kwa muda sasa na hata mazingira ya shule si ya kuridhisha.

Afisa elimu amesema shule hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa ada za wazazi na wazazi wamekuwa halipi ada kwa wakati hali iliyopelekea walimu kutolipwa mishahara yao hivyo wamekuwa hawaingii madarasani.


Mpya zaidi Nzee zaidi