Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa miezi miwili kwa wafanyabiashara wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajiliwa wajitokeze kufanya usajili haraka
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Frank Kanyusi amesema katika elimu ya urasimishaji biashara ambayo inaendelea kutolewa na wakala huo mikoani, imebainika kuwepo kwa wafanyabiashara wengi wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajili ambapo sheria ya majina ya biashara inamtaka mfanyabiashara kusajili jina la biashara yake ndani ya siku 28 toka aanze kulitumia na kwamba kinyume na hapo atakuwa amevunja sheria ya majina ya biashara.
Kwa sasa Usajili wa majina ya biashara umerahisishwa kwani unafanywa kwa njia ya mtandao hivyo ni wafanyabiashara kutembelea tovuti ya BRELA ambayo ni www.brela.go.tz watapata maelezo yote ya namna ya kusajili jina la biashara.
BRELA inawajibu wa kuhakikisha biashara zinarasimishwa nchini ili serikali iweze kuwatambua walipa kodi wake na kwa kufanya hivyo watachangia pato la taifa kukua na kuifanya nchi hii kuwa ya uchumi wa kati ifika mwaka 2025.