Yasmani Duk: Anayeamini Neymar alistahili kiwiko



Neymar
Ijumaa Neymar (24), alishindwa kuendelea na mpira baada ya kupigwa kiwiko na mchezaji wa Bolivia, Yasmani Duk, wakati wa mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Neymar ambaye katika mchezo huo alifunga bao lake la 300 tangu aanze kucheza soka, kiwiko hicho cha Duk kilitua upande wa kulia juu ya jicho na kumchana vibaya hivyo kumsababishia kuvuja damu nyingi.

Hata hivyo, wakati ulimwengu wa soka ukitarajia kwamba Duk angeomba msamaha kwa kosa alilolifanya, mchezaji huyo wa Bolivia amekataa kuomba msamaha kwa nyota huyo wa Barcelona huku akidai alistahili kiwiko hicho.

Wakati vyombo vingi vya bahari vikimtupia lawama Duk kwa kutokuwa muungwana, mchezaji huyo ameeleza kuwa kitendo hicho ni kama sehemu na mzigo wa mchezo, huku akimshambulia Neymar.

"Neymar alikuwa mbinafsi sana- alikuwa kama hivyo kwetu sote kwa muda wote wa mchezo, lakini kwa jumla nilichojaribu ni kuzima hekaheka zake kukimbia – kitu ambacho kinatokea katika soka. Kila mtu anajua mchezo unasehemu ya mwili.

“Niliwahi kuvunjika pua hakuna aliyetoa neno lolote," alifafanua Duk, ambaye pia alitenga nafasi ya kumshauri Neymar:

"Kuwa mchezaji bora wa dunia, anapaswa kuacha B******s' tabia, anza kuonyesha kujali wapinzani."
Hivyo ndivyo Duk alivyoonyesha kutojali kwa kumuumiza Neymar katika mechi hiyo ambayo Brazil ilipiga mtu mkono (ilishindi mabao 5-0).

Duk aliyezaliwa miaka 28, iliyopita huko Santa Cruz de la Sierra, Bolivia anacheza nafasi ya ushambuliaji, kwa sasa anakipiga kwa mkopo New York Cosmos akitokea Boys Warnes ya nyumbani kwao.

Kwa upande wa Neymar, ambaye hilo ni bao lake la 49 kwa timu ya taifa alishindwa kuendelea na mpira katika dakika ya 69.
Ameshafunga mabao 95 tangu alipojiunga na Barcelona, huku akitupia 138 wakati akiwa Santos.
Mpya zaidi Nzee zaidi