KATIKA kukabiliana na kasi ya maambukizi ya UKIMWI katika halmashauri ya manispaa ya Iringa, baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo wameshazishauri kamati za UKIMWI za kata kuongeza juhudi katika zoezi la utoaji wa elimu kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo sambamba na kupiga marufuku uvaaji wa nguo fupi maarufu kama ?vimini? miongoni mwa watoa huduma katika maeneo yanayouza vileo.
Akichangia taarifa ya kamati ya UKIMWI mbele ya baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, diwani wa kata ya Mshindo Bw. Ibrahimu Ngwada amesema kumekuwa na mmonyoko mkubwa wa maadili miongoni mwa wana jamii kiasi ya kwamba ktk maeneo mengi ya kuuza vileo wahudumu wamekuwa wakivaa nusu utupu hali ambayo ameilezea kuwa ni kama bomu linalosubiri kulipuka.
Kwa upande wake Mratibu wa UKIMWI wa manispaa ya Iringa Bi Dora Myinga akataja mikakati ambayo ofisi yake imekuwa ikiichkuwa kupambana na janga la UKIMWI huku diwani wa kata ya Gangilonga Bw Dady Igogo akionesha takwimu za kata yake namna ilivyoathirika na UKIMWI.
