VIDEO: Sababu za benki kulalamika kufilisika wakati huu

Leo November 30 2016 msajili wa hazina, Lawrance Mafuru amekutana na waaandishi wa habari, pamoja na mambo mengine suala aliloligusia ni pamoja na benki nyingi nchini kulalamika kufilisika wakati huu ambapo serikali imeamua fedha zake kuziweka benki kuu na kuzitoa katika mabenki ya biashara.

Mafuru ameeleza kuwa kufilisika kwa mabenki ni kutokana na kukopesha zaidi ya trilioni 1.4 kwa watu huku madeni hayo kutokuwa na uhakika wa kulipwa na sio pesa za serikali zilizopo benki kuu kwa sasa. 

Mpaka mwezi september sekta ya mabenki imekopesha zaidi ya trilioni 17, hiyo ni mikopo ambayo watanzania, sekta za umma wamekopa, kwenye mikopo hiyo 9% au trilioni 1.43 ni mikopo mibovu maana yake kuna watu wamekopa pesa hazijarudi’