F Wanafunzi 3 wamekufa baada ya kuzama wakiogelea katika ziwa Tanganyika mkoani Kigoma. | Muungwana BLOG

Wanafunzi 3 wamekufa baada ya kuzama wakiogelea katika ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.

Wanafunzi watatu ,wawili wakiwa wa shule ya msingi na mmoja wa sekondari wamekufa baada ya kuzama katika ziwa Tanganyika wakati wakiogelea katika ufukwe wa ziwa hilo mjini Kigoma.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi  Ferdinand Mtui amewataja wanafunzi hao kuwa ni Omar Ramadhan mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Kipampa na Haiman Kalenga mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Livingstone.

Mwanafunzi mwingine ni Hussein Moshi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Rusimbi katika manispaa ya Kigoma Ujiji, amesema wanafunzi hao walipatwa mauti baada ya kuzama wakati wakiogelea katika eneo la Rutale katika ziwa Tanganyika jana jioni.

Kamanda Mtui amesema maiti za marehemu hao zimepatikana na kuhifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Kigoma Maweni.