BAADA ya kusitisha ajira za umma kwa takribani miezi tisa, Serikali imesema katika mwaka huu wa bajeti itaajiri watu 71,496 kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu, afya na viwanda.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na Nipashe juu ya lini Serikali itaanza kutoa ajira, baada ya kuzisitisha kwa muda, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Florence Temba, alisema Serikali inatoa fursa za ajira kama ilivyoelezwa katika mpango mwaka wa fedha 2016/17.
Katika majibu hayo aliyoyatoa kwa niaba ya Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, yalibainisha kwamba ajira hizo zitakuwa kwenye sekta ya elimu, afya, kilimo na mifugo.
