Moze Iyobo akiwa na Aunt Ezekiel
Msanii wa filamu nchini Aunt Ezekiel amedai kuwa anatamani tena ajifungue mtoto wa kike kwa mara ya pili kwani watoto wa kike kuwa nao ni pesa.
"I wish nipate mtoto wa kike tena, watoto wa kike hela ile, yaani mpaka wajae" alisema Aunt Ezekiel
Mbali na hilo Aunt Ezekiel anakiri kuwa kwa wanaume wote aliokuwa nao hakupata kitu cha maana ila toka amekuwa na mzazi mwenzake ambaye ni Moze Iyobo anaona kuna mambo mengi ya maendeleo ambayo ameweza kufanya, hivyo Moze amembadilisha sana maisha na kumfanya apige hatua za maendeleo.
"Kuwa na Moze Iyobo kumenipeleka mbele sana kimaendeleo, kote nilikopita sijapata kitu cha maana" alisema Aunt Ezekiel kwenye Friday Night
