Msanii Shilole
Msanii wa muziki wa bongo fleva Shilole amefunguka na kusema kuwa mafanikio yake aliyopata kwenye muziki kama angeendelea kufanya filamu anaamini asingeweza kuyapata kabisa.
"Namshukuru Mungu nimefikisha miaka 28 najivunia mafanikio yangu katika umri huu nilionao, nashukuru kweli kwani tayari nina bonge la mjengo na miaka yangu 28, nina watoto wawili, na biashara zingine za hapa na pale ikiwepo biashara ya chakula" alizungumza Shilole
