Chanzo cha moto Shule ya Sekondari Ufundi kuchunguzwa

Askari wa jeshi la zimamoto wakishirikiana na askari wa jeshi la polisi kuzima moto uliokuwa ukiunguza bweni la shule ya Ufundi Mtwara. Picha na Haika Kimaro 

Mtwara. Baada ya bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Ufundi kuteketea kwa moto, polisi mkoani Mtwara imeanza uchunguzi.

Katika tukio hilo lililotokea juzi saa moja asubuhi, hakuna aliyejeruhiwa kwa kuwa baadhi ya walimu kutoka shule mbalimbali mkoani hapa waliokuwa wakilitumia hawakuwamo ndani na wanafunzi wapo

likizo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Thobias Sedoyeka amesema hakuna madhara kwa binadamu na kueleza chanzo cha moto huo kinachunguzwa na taarifa zitakapokuwa tayari zitatolewa.

Mmoja wa walimu aliyekuwa katika semina shuleni hapo, Masele Francis amesema waliona moshi ukitoka katika bweni hilo na walipofuatilia waligundua kuwa kuna moto na kitu walichofanya ni kufuatilia kama kulikuwa na watu ndani ndipo walipobaini kwamba mwenzao mmoja alikuwa bafuni na kumuokoa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha