Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, imesikiliza shauri la mgogoro wa mipaka ndani ya Msitu wa Kazimzumbwi wilayani Kisarawe.
Mahakama juzi ilionyeshwa nguzo zilizowekwa kuonyesha mipaka ya msitu huo uliotangazwa kuwa hifadhi 1954 na mahali ambako wadai walihamishwa wakidaiwa kuvamia msitu.
Hatua hiyo ililenga kujionea uhalisia wa mipaka ya msitu huo inayobishaniwa mahakamani kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na wananchi wa vijiji vya Nzasa na Kimwani.
Kesi hiyo ya ardhi namba 237 ya 2012 ilifunguliwa na Boniface Makunja na Waziri Njau kwa niaba ya wenzao 237 wanaodai walikuwa wakazi wa vijiji vya Nzasa na Kimwani, Kata ya Chanika wilayani Ilala, kabla ya kuhamishwa kwa kuchomewa nyumba zao 1998.
Wadaiwa katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii; Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wanaowakilishwa na Wakili wa Serikali, Benson Hossea.
Wananchi hao wanadai fidia ya Sh5.7 bilioni kwa kuchomewa nyumba na mazao yao huharibiwa wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika makazi yao kwa nguvu iliyojulikana ‘Operesheni Okoa Kazimz