Baraza la habari Tanzania – MCT limelaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa ITV Halfani Lihundi kwa kisingizio cha uchochezi, na kueleza hayo ni matumizi mabaya ya madaraka ambayo hayawezi kukubalika.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara, katibu mtendaji wa baraza hilo Kajubi Mukajanga amesema, kwa kipindi sasa kumeanza kuonekana hali inayoendelea ya waandishi wa habari kutiwa ndani, na ingawa baraza linatambua wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanayo sheria ya kumweka mtu ndani, lakini tatizo ni namna sheria hiyo inavyotumika, kwani viongozi huacha kufuata taratibu za kupeleka malalamiko, na badala yake hukimbilia kumweka mwandishi ndani, na kusisitiza, hali hiyo haiwezi kukubalika ya kutumika kwa sheria ya uchochezi, kuwageuza waandishi wa habari kama watenda makosa ya jinai.
Aidha amewataka viongozi kuelewa kuwa waandishi wa habari sio maadui wanapofichua maovu na malalamiko ya wananchi na badala yake wayafanyia kazi, kwa kuwa serikali ya awamu ya 5 ya rais John Magufuli imejipanga kupambana na vitendo vya ukosefu wa maadili, kama rushwa wizi, uzembe na matumizi mabaya ya rasilimali.