Serikali kuwawezesha walemavu wasioona wanaoshona nguo.

Serikali imeelezea kufurahishwa kwake na uwepo walemavu wasioona wanaoshona nguo ambao wanashiriki maonesho ya viwanda vya ndani huku wakionesha kwa vitendo wanavyofanya shughuli hiyo na imeahidi kuwasaidia walemavu wa namna hiyo nchini ili wajikwamue kiuchumi.

Waziri wa fedha na mipango Dr. Philip Mpango amesema hayo katika banda la maonesho ya walemavu wasioona wanaoshiriki maonesho hayo ya viwanda vya ndani na kuwaomba wenye viwanda vya nguo pamoja na wahisani kujitokeza kuwasaidia walemavu hao wasioona waweze kujitegemea kiuchumi.

Katika maonesho hayo ya kwanza ya viwanda vya ndani, kada mbalimbali zimetumia nafasi hiyo kupata elimu ya ujasirimali pamoja na jinsi ya kuweza kufanya uchaguzi wa biashara ya kufanya ama mafunzo ya kusomea ambayo yana soko katika ajira.

Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo na watu waliofika kujionea yanayojiri wamesema wameweza kutimiza malengo yao kwa kuwepo watu wengi wanaofika kujionea sambamba na huduma mbalimbali zinazohitajika katika maonesho kama hayo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items