Jeshi la polisi wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya kundi kubwa la wachimbaji madini ya Dhahabu wadogowadogo waliovamia mgodi wa muwekezaji kwa madai kuwa eneo hilo wamelivumbua tangu mwaka 2008 hadi mwaka 2014 walipoondolewa na kukabidhhiwa ushirika wa Isinka.
Kama unavyojionea askari polisi wakiimalisha ulinzi kudhibiti kundi kubwa la wachimbaji madini ya dhahabu wakiwa katika mgodi Isinka wa Ishokela hela ambapo wameiomba serikali kuwarejeshea eneo lao lenye ukubwa wa hekta 2250 zilizohodhiwa na muwekezaji katoni Kitonga Company Limited tangu mwaka 1990 bila kuendelezwa ili waweze kuondokana na uvamizi wa maeneo ya wawekezaji likiwemo eneo la ushirika wa Isinka Ishoikela hela linalomilikiwa na wachimbaji 104.
Akijibu malalamiko hayo katibu wa mgodi wa Isinka Federation Ishokela Hela Bw. John King Balole amesema kuwa mgodi huo wenye hekta 20 unamiliokiwa na wachimbaji 104 kisheria wakiwa na leseni ya uchimbaji.
Uchunguzi wa ITV umebaini hekta 2250 zilizohodhiwa na muwekezaji Katoni Kitonga Company Limited tangu mwaka 1990 bila kuendelezwa ambaye kwa sasa hayupo nchini akiwa ameacha ulinzi katika eneo hilo kwa lengo la kudhibiti wavamizi wasijihusishe na uchimbaji wa madini kwenye eneo.