Ufunguzi wa Kongamano la SHILO Watanzania wasisitizwa kudumisha amani

Watanzania wamesisitizwa kudumisha amani na utulivu uliopo nchini, ili kuipa nafasi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kutimiza malengo yake ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Msisitizo huo wa amani umetolewa jijini Dar es salaam na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni jijini Dk.Getrude Rwakatare wakati alipokuwa akizungumza na waandisjhi wa habari kwenye ufunguzi wa kongamano maalumu la Shilo ambalo huendeshwa kwa siku takriban nane mfululizo.

Aidha, Mchungaji huyo amewataka Watanzania kujikabidhi kwa Mwenyezi Mungu wakati wanapomaliza mwaka ili awasaidie kuilinda na kuidumisha amani yao, ikiwa ni pamoja na kuomba maaada wa Mungu katikam kuunza mwaka mpya.

Kwa mujibu wa Dk. Rwakatare, siku ya kwanza kabisa ya kongamano hilo huwa ni maalumu kwa ajili ya maombezi ya taifa.