Handeni. Wakazi wa wilayani hapa Mkoa wa Tanga, wamesema kuwa wanategemea maembe ili kuishi kutokana na kushindwa kupata chakula kwenye maeneo yao.
Walitoa kilio hicho kwa Mbunge wa Handeni Vijijini, Mboni Mhita walisema mahindi hayaonekani na yakipatikana bei yake ni kubwa.
Mkazi wa Kijiji cha Kwamwenda, Rashid Madanga alisema wananchi wanalazimika kutegemea maembe kama chakula chao kwani mahindi hayaonekani na yanayopatikana bei yake ni kubwa.
Diwani wa Ndolwa, Joel Mabula amesema: “Kilo ya mahindi ni Sh1,000 huku gunia limefikia mpaka laki moja siyo wananchi wote wanaweza kununua hicho chakula, hivyo nakuomba mbunge ulione hilo.”