Wasafiri wa mikoani waadimika Ubungo

Dar es Salaam. Idadi ya wasafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo (UBT), imepungua ikilinganishwa na mwaka jana.

Hali ya usafiri katika kituo hicho ni ya kawaida, tofauti na miaka ya nyuma ambako kwa kipindi kama hiki mabasi huadimika kutokana na wingi wa abiria.

Katibu wa Chama cha Mawakala wa Mabasi Ubungo (CMU), Rashid Mchomvu amesema hata kwa mikoa ambayo huwa inaoongoza kwa kuwa na abiria wengi kipindi hiki kama Arusha, Kilimanjaro na Mwanza abiria wamepungua.

“Mwaka jana tarehe na mwezi kama huu gari zilikuwa zikijaza, pia abiria walikuwa wengi, mwaka huu unaweza kuondoka na abiria 40 hadi 50 jambo ambalo hatukulitegemea... hali inaonekana tofauti pengine tusubiri tarehe za katikati na mwishoni, upepo unaweza kubadilika,” alisema.

Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji, amesema hali ya usafiri haijachanganya.

“Hakuna shida ya usafiri kwa sasa, abiria si wengi kama inavyoelezwa kuwa mwezi kama huu abiria huwa wanakuwa wengi, pengine tusubiri mpaka mwishoni au katikati ya mwezi,” amesema  
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items