F Watoto waporwa ng’ombe machungani | Muungwana BLOG

Watoto waporwa ng’ombe machungani

Kibiti. Watu wanaodaiwa kuwa majangili wakiwa na silaha wamepora ng’ombe 35 wakiwa malishoni katika Kijiji cha Nyamisati wilayani hapa.

Pia, waliua ng’ombe sita na kuwajeruhi wengine tisa kwa kitu chenye ncha kali.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gullamhusein Kiffu alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa saa tisa alasiri. Alisema ng’ombe hao waliporwa kutoka kwa watoto wawili waliokuwa wakiwachunga.