F Watumishi kudhibitiwa kwa CCTV | Muungwana BLOG

Watumishi kudhibitiwa kwa CCTV

Korogwe. Ili kuwadhibiti watumishi wanaotumia simu muda wa kazi, Wizara ya Afya ina mpango wa kufunga kamera maalumu (CCTV) kwenye hospitali za wilayani.

Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu alisema hayo juzi wakati wa ufunguzi wa kituo cha redio cha Voice Of Africa wilayani Korogwe.

Alikuwa akijibu swali la mtangazaji wa kituo hicho aliyetaka kujua Serikali itadhibiti vipi tatizo la watumishi na hasa wa wizara hiyo wanaokiuka maadili kwa kuchezea simu muda wa kazi.