YANGA imevuna faida ya mgomo baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Lyon walitangulia kwa bao la Ludovic Venance dakika ya 67 akimalizia pasi ya Abdallah Mguhi ‘Messi’, kabla ya Mrundi Amissi Tambwe kuisawazishia Yanga dakika ya 74 akimalizia krosi ya Juma Abdul.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Saidi Juma, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke.
African Lyon; Jehu Youthe, Miraj Adam, Baraka Jaffary, Halfan Twenye, Hamadi Waziri, Hamadi Manzi, Hassan Isihaka, Omary Abdallah, Awadh Juma, Thomas Maurice na Abdallah Mguhi.