Zaidi ya shilingi Trilioni tano kutumika kuboresha miundombinu ya umeme nchini.

Zaidi ya shilingi Trilioni tano zinatarajiwa kutumika katika miradi ya uboreshaji wa miundombinu ya umeme ukiwemo mradi mkubwa na kwanza tangu uhuru ambao utasambaza umeme zaidi ya mikoa kumi na utatumia shilingi trilini 1.02.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Eng. Felchesmi Nramba mara baada ya kutembelea na kukagua hali ya miradi minne mikubwa inayotekelezwa hapa jijini kikiwemo kituo cha Muhimbili ambacho kitatumika maalum kwa hospitali ya Taifa Muhimbili na taasisi zake ili iondokane na kero ya umeme inayokabiliana nayo.

Kuhusu mradi wa kusambaza umeme mikoa zaidi ya kumi utakaoanzia mkoa wa Iringa hadi Mwanza Bw Mramba amesema umekamilika kwa asilimia 99 na unatarajiwa kufunguliwa na Rais Magufuli mwezi Januari mwaka huu.