Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kuwania kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe hilo, Yanga wapokea kichapo cha bao 4-0 kutoka kwa Azam FC licha ya timu zote mbili kufuzu na kuingia hatua hiyo.
Katika hatua ya nusu fainali Yanga alikutana mtani wake wa jadi, Simba siku ya Jumanne na Simba kufanikiwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kutoka suluhu ndani dakika 90 za uwanjani hivyo kuwaondoa kwenye mashindano hayo.
Baada ya kipigo hicho Yanga walishambuliwa mitandaoni na watani wao wa jadi (Simba) kwa kipigo hicho na kile cha Azam kilichopewa jina la 4G.