Basi la gonga mwendesha Pikipiki na kupinduka

Mwendesha pikipiki mkazi wa babati mjini mkoani Manyara amefariki dunia muda mchache baada ya kugongwa na basi la Nkondo katika eneo la mwisho wa lami mjini babati na kusababisha abiria zaidi ya 50 waliokuwa wakisafiri na basi hilo kunusurika kifo kufuatia basi hilo kupinduka huku abiria 5 wakijeruhiwa baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulidhibiti basi lake.

Ajali hiyo iliyohusisha basi hilo la Nkondo lenye No. za Usajili T 936BMK kutoka mkoani Mwanza kueleka mkoani Arusha ,muda mfupi bada ya kutokea kwenye kituo cha mabasi cha mjini Babati,huku baadhi ya abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo wakisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi  kutaka kumpita dereva wa pikipiki ambae ghafla alichukua uamuzi wa kuelekea upande wa kulia.

Nae Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Manyara Bi. Mary Kipesha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  na kudai chanzo ni mwendo kasi wa dereva huyo huku  ni mkuu wa wilaya ya Babati Bw.Raymondi Mushi akielezwa kushangazwa  na matukio ya ajali za pikipiki yanavyoongezeka mjini Babati ilhali serikali imetoa mafunzo ya udereva mara kadhaa.
Mpya zaidi Nzee zaidi