Mkuu wa Mkoa wa Mwanza awasimamisha kazi watendaji waandamizi

????????????????????????????????????
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela, amewasimamisha kazi watendaji wa ngazi za juu katika Halmashauri ya wilaya ya Magu mkoani humo, ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya zaidi ya shilingi millioni mia tatu, zilizotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya maendeleo baada ya kinachdaiwa kufanya mabadiliko bila bila kuihusisha Wizara ya fedha na mipango.

Waliosimamishwa kazi ni Mweka hazina, mchumi pamoja na Mhandisi wa Halmashauri hiyo, baada ya kubadili matumizi ya fedha za kutekeleza miradi ya SEDEP, zilizotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Katika ziara hiyo ya Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ya Magu mkoani Mwanza Hadija Nyembo, akaeleza mambo yaliyokwamisha miradi ya SEDEP, na kuthibitiwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Magu George Lutengano.

Kutokana na sababu hizo mkuu huyo wa mkoa, akagoma kwenda kuzindua vyumba viwili vya Madarasa vya shule ya Sekondari Nyanguge vilivyojengwa kupitia kiasi hicho cha fedha, kutokana na madai kuwa vyumba hivyo pamoja na ujenzi wa vyoo vimejengwa chini ya kiwango.
Mpya zaidi Nzee zaidi