Dar es Salaam. “Huu ni mradi mkubwa zaidi Afrika, nchi tatu pekee ambazo zinao, lakini nina uhakika ukikamilika kwa awamu zote sisi ndiyo tutakuwa vinara, tuutunze watu wa mataifa mengine watakuja kujifunza kwetu.”
Kauli hiyo aliitoa Rais John Magufuli wakati akizindua mradi wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam (Dart) na siku mbili baadaye inaonekana kutimia baada ya ujumbe wa watu 10 kutoka Serikali ya Zimbabwe kutua nchini kujifunza kuhusu usafiri huo.
Ujumbe huo uliongozwa na Waziri wa Kazi, Nyumba na Serikali za Mitaa wa Zimbabwe, Savior Kasukuwere na watendaji wengine wa Serikali na mji wa Harare.
Waziri Kasukuwere alisema Zimbabwe imevutiwa na mradi huo na ina mpango wa kuutekeleza mjini humo ili kukabiliana na changamoto ya usafiri na msongamano wa magari uliopo sasa.
Alisema ameona namna Dar es Salaam ilivyoanza kubadilika na hilo linaweza kutokea pia Harare kwa kuwa ni miji inayofanana.
“Harare haina tofauti na Dar es Salaam, tuna changamoto ya usafiri ndiyo maana tukaona tuje kujifunza hapa mazingira yetu yanaendana tofauti na Nigeria na Afrika Kusini ambao pia wana mradi huu,” alisema Kasukuwere
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema kuanza kwa mradi huo ni mafanikio na sifa kwa Tanzania.
“Tukiacha faida za kiuchumi na kuondoa msongamano, mradi huu unatupa sifa Watanzania, tujivunie watu wanakuja kujifunza kutoka kwetu,” alisema Simbachawene.
Msafara huo ulipanda mojawapo ya mabasi hayo ili kuona yanavyofanya kazi. Safari ilianzia Kivukoni hadi kituo cha Ubungo Maji.