Ndege ya Urusi yawaua wanajeshi wa Uturuki Syria

 Rais wa Urusi Vladimir Putin ameomba msamaha baada ya shambulizi la Urusi kuwaua kimakokosa wanajeshi watatu wa Uturuki kaskazini mwa Syria.

Wanajeshi hao walikuwa wakiwasaidia waasi nchini Syria, wakati wa jitihada za kuuteka mji wa al-Bab kutoka kwa kundi la Islamic State.

Hi ni sehemu ya hatua kubwa inayofanywa na Uturuki kuwatimua Islamic State, mbali na mpaka wa kusini mwa Uturuki.

Urusi na Uturuki ambao wanaunga mkono pande pinzani wamekuwa wakiwapiga vita Islamic State hivi majuzi kwa mashambulizi ya ndege.


Mpya zaidi Nzee zaidi