Tundu Lissu agoma kula

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema kuwa wao kama chama pamoja na familia ya Mbunge Tundu Lissu wamekubaliana na kuridhia mbunge huyo kufanya mgomo wa kutokula chochote hadi hapo atakapofikishwa mahakamani.

"Mhe Lissu ameendelea kushikiliwa na Polisi bila kufikishwa mahakamani. Hajafunguliwa mashtaka yeyote hadi sasa na Polisi wameendelea kumkatalia dhamana. Unyanyasaji huu dhidi wa wawakilishi wa wananchi na viongozi wengine wa chama unatia doa kubwa demokrasia katika nchi yetu. Baada ya mashauriano na Mhe Lissu na familia yake, chama kimeridhia na kimeafiki Mhe. Lissu kuanza rasmi mgomo wa kula chochote (hunger strike) hadi hapo atakapofikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka rasmi" alisema Freeman Mbowe

Mbali na hapo Freeman Mbowe amewataka watanzania kuendelea kumuombea kiongozi huyo na kuijaza faraja familia yake pamoja na viongozi mbalimbali wanaopambana na changamoto mbalimbali.






VIDEO; MAAJABU JAMAA  ANAECHEZA NA  NYUKI