Wafanyabiashara Mbeya Kizimbani Wakabiliwa na Mashitaka ya Uhujumu

Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabilisa watu saba, akiwemo Afisa mmoja wa TRA na Mfanyabiashara Maarufu wa Samaki Jijini Mbeya Josephate Mushi, imetajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya na kuahirishwa baada ya Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Akisoma kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba mbili ya mwaka 2017 Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya Michael Mteite, anasema washitakiwa wote saba kati ya Desemba 22 mwaka jana, na Januari 22 mwaka huu Jijini Mbeya, kwa pamoja wamesaliti na kumiliki bidhaa aina ya samaki mbazo hazijalipiwa kodi,na kuziingiza nchini zikitokea nchini China zenye thamani ya shilingi milioni 206 bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Samaki.

Wahitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka Manne ,shitaka la kwanza hadi la tatu likiwa ni kuongoza na kupanga uhalifu na shitaka la nne ni kukutwa na bidhaa ambazo hazijalipiwa kodi.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote mahakani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza mashitaka hayo wala kutoa dhamana .

Aidha Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo akinukuu kifungu cha 29, kifungu kidogo cha sheria namba 4 D, anasema kifungu hicho kinasema kwenye kesi ya uhujumu uchumi, thamani ya kitu chochote ama bidhaa inayokamatwa yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 Mahakama yenye Mamlaka ya kusikiliza na kutoa dhama ni Mahakama kuu pekee.

Mahakama imewashauri Mawakili wa upande wa utetezi kuomba Rufaa ya Shauri hilo Mahakama kuu ,ambapo imewarejesha tena mahabusu washitakiwa na kesi hiyo itatajwa tena Februali 23 mwaka huu.

Washitakiwa hao ni Josephate Mushi ambaye ni Mfanyabiashara maarufu wa Samaki Jijini Mbeya, Said Sisige, Agripa Benjamini, Andrew Ngachengo, ambaye ni Afisa wa TRA, Pius Joseph, Said Ramadhani na Shaabani Sankwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi