Barcelona wavunja mazungumzo ghafla

Hispania. Klabu ya Barcelona imesitisha majadiliano dhidi ya timu ya Athletic Bilbao kuhusu kumnunua kocha Ernesto Valverde ambaye alitarajiwa kumrithi Luis Enrique.

Valverde amekuwa akihusishwa kwa ukaribu zaidi kuhamia kwenye dimba la Nou Camp baada ya Enrique  kutangaza rasmi nia yake ya kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari Hispania zinasema kwamba  Barcelona ilisema kwamba kulikuwapo na mazungumzo ya awali kuhusu kocha huyo mwenye miaka 53 kukinoa kikosi hicho, hata hivyo mabingwa hao wa Kombe la Mabingwa Ulaya wamevunjwa mazungumzo hayo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items