Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe imeigawia jamii ya wafugaji jumla ya vijiji 24 kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kifugaji, lengo likiwa kupunguza mgogoro baina ya wakulima na wafugaji wilayani humo.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara na jamii ya wafugaji kwenye kijiji cha Mzenga, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda amewataka wafugaji wilayani huo kuachana na ufugaji wa kuhamahama na kufanya ufugaji wa kiuwekezaji, ikiwa ni pamoja na kujenga makazi ya kudumu na kuwapeleka watoto shule.
Jamii ya wafugaji wilayani Kisarawe imekuwa ikilaumiwa mara kwa mara kuwa ndiyo chanzo cha mgogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa madai ya kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa chama cha wafugaji Tanzania bwana Maghembe Makoye ameitaka jamii ya wafugaji wilayani Kisarawe kutumia vizuri fursa waliyopewa ya maeneo ya ufugaji na kufanya ufugaji wa kisasa na kuachana na ufugaji wa kuhama hama.
Aidha, amezitaka halmashauri nyingine kuiga mfano wa Kisarawe wa kuwatengea maeneo maalumu wafugaji kwani huo ndiyo muarubaini wa kuondoa migogoro baina ya wakulima na wafugaji.