Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii walilazimika kushuka na kuzungumza na wananchi hao.
Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pi ni jummbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Godwin Mollel akizungumza na wananchi wa jamii ya Wafugaji katika kijiji cha Mbukeni baada ya kuzia safara wa kamati hiyo.
Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukeni,Kata ya Harashi ,tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro jana wamezuia kwa muda msafara wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakishinikiza kusikilizwa kero zao.
Katika Pori tengefu la Loliondo lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kumekuwa na mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa huku suluhu ya utatuzi wa kiini cha mgogoro huo kikitafutiwa ufumbuzi.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii imetembelea maeneo mbalimbali ya Pori hilo kwa lengo la kujionea hali halisi kabla ya kutoa tamko juu ya mgogoro huo ambapo ikiwa njiani kuelekea Mamlaka ya Ngorongoro ikakutana na kundi la wafugaji wakiwa wamezuia barabara
Hatua ya wafugaji hao kusimamisha msafara wa kamati inakuja muda mfupi baada ya kamati kufanya kikao na wawakilishi wa wafugaji hao,kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Domel.