Khalid Chokoraa: Mziki wa Singeli haujanishinda

Msanii Khalid Chokoraa aliyekuwa anafanya vizuri katika miondoko ya dansi amekanusha zile tetesi ya yeye kufeli muziki wa singeli na kusema hakuna ukweli katika hilo kwa sababu kazi zake mpaka sasa zimepata mapokezi mazuri pamoja na ‘airtime’.

Akiongea kupitia kipindi cha eNewz Chokoraa amesema hawezi kushangazwa na hayo maneno kwa kuwa kila kitu ni mipango huku akisisitizia watu wawe na subira watamuelewa anachokifanya japokuwa itachukua muda mrefu.

“Mimi malengo yangu yanaenda vizuri kwa sababu kila kitu ni mipango tu, huwezi kuwa na 10 bila ya kuanza moja kwa hiyo tunaenda vizuri kwenye muziki wa singeli, nimeshaachia nyimbo mbili mpaka sasa,  ya kwanza inaitwa ‘Baba mwenye nyumba’ na ya pili nimefanya na Kalala Junior. Tunajiita watoto wa nje ya ndoa”. Alisema Chokoraa

Pamoja na hayo msanii huyo amesema yeye amezaliwa ndani ya ndoa ila ameamua kutumia jina la watoto wa nje ya ndoa kama mwamvuli kwa watu wanaomzunguka ambao hawajapatikana katika mchakato wa halali.

Kwa upande mwingine Chokoraa amesema hana mpango wa kutoa albam kama wasanii wengine ila yeye ataendelea na ule utamaduni wa kuachia ‘ngoma’ kisha kufanya ‘show’ kwa madai kuwa albam hazilipi