Museveni atishia kuingia Congo kuwasaka waasi wa ADF.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametishia kuingia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwasaka Waasi wa Allied Democratic Forces ADF,anaodai wanahusika katika mauaji nchini Uganda.

Museveni pia ametishia kupunguza idadi ya wahudumu wa boda boda jijini Kampala, akisema wahudumu hao Sasa wanatumika na wahalifu.

Rais Museveni ameziamuru mamlaka jijini Kampala kueka kamera za CCTV katika jiji lote ili kiwanasa wahalifu kwa haraka,akisema hiyo ndiyo mbinu ya kisasa inayotumika katika Nchi Na miji iliyoendelea kama New York. Kwake Museveni,mbinu zinazotumika kukabiliana Na wahalifu nchini Uganda ni za zamani, ikiwa pamoja Na kuulizia walioshuhudia.

Akitumia lugha yenye matusi mazito kwa lugha ya kiingereza, Museveni anasema mauaji ya watu wa vyeo vya juu ni wazembe Na anahisi kwamba baadhi ya maafisa wake wa usalama wanahusika katika kutekeleza uhalifu.

Museveni ametoa maagizo kwa maafisa wake walio Museveni anasema maafisa wa usalama hawaaminiki na raia walio Na taarifa muhimu kuripoti wahalifu.

Museveni anadai kwamba baadhi ya polisi wake ni majambazi,na kuwataka polisi kujichunguza akisema ana imani kwamba polisi wanaua raia.