Simbachawene astukia hila uhakiki wa vyeti

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene 

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewataka watumishi wa umma waliositishiwa ajira zao kimakosa wakati wa uhakiki wa vyeti wapeleke vielelezo vyao Tamisemi.

Simbachawene aliyasema hayo jana Jijini Arusha alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa wadau wa mfuko wa pensheni wa LAPF.

Simbachawene alisema baadhi ya watendaji wasiokuwa  waaminifu kwa makusudi, wamesitisha ajira za baadhi ya watumishi wenzao kwa kutumia mgongo wa uhakiki wa  vyeti.

Alitoa rai kwa watumishi hao kufika  haraka kwenye ofisi za Tamisemi wakiwa na nyaraka zitakazosaidia kuwarejesha kazini.

“Kuna baadhi ya watendaji waliokuwa wakifanya uhakiki wa vyeti  vya wafanyakazi hawakutenda haki, yao walionewa katika uhakiki huo, hivyo nawaomba wafike ofisi za Tamisemi wakiwa na vielelezo vyao,” alisema Simbachawene.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items