https://monetag.com/?ref_id=TTIb Taifa Stars ailaza Burundi 2-1 | Muungwana BLOG

Taifa Stars ailaza Burundi 2-1

Taifa Stars imeendeleza ushindi baada ya kuitwanga Burundi katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars inashinda mechi ya pili mfululizo baada ya kuitwanga Botswana kwa mabao 2-0, Jumamosi iliyopita.

Huku ikicheza bila nahodha wake, Mbwana Samatta ambaye amerejea mapema Ubelgiji kujiandaa na michuano ya Europa League, ilionyesha kiwango kizuri.

Ushindi wa leo haukuwa rahisi kutokana na umahiri wa wachezaji wa Burundi wakiongozwa na Laudit Mavugo.

Stars liana kupata bao lake la kwanza kupitia Simon Msuva ambaye aliunganisha krosi ya Mohamed Zimbwe iliyotua kichwani mwa Ibrahim Ajibu kabla ya kumfikia mchungaji.

Mavugo aliisawazishia Burundi akimhadaa Deogratius Munishi aliyetoka langoni mapema.

Lakini Mbaraka Yusuf anayetokea Kagera Sugar, ikiwa ndiyo anaanza kuichezea Stars, akafunga bao zuri kabisa baada ya mpira wake wa kwanza kugonga mwamba, lakini akamalizia kwa shuti la mguu wa kushoto.


Juhudi za Burundi kukomboa au Taifa Stars kuongeza, hazikuzaa matunda hadi mwisho wa dakika 90.