Tani 3,000 za mchele zazuiwa kuuzwa Dar

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limesema mchele unaotoa harufu uliongizwa jijini Dar es Salaam na kuanza kusambazwa ni tani 3,000.

Mchele huo umekutwa kwenye mifuko 1,058 ya kilo 25 kila mmoja katika ghala lililopo eneo la Majumbasita -Ukonga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema polisi walifanikiwa kufika katika ghala hilo wakiwa na maofisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kuzuia usambazaji wake.

Kwa upande wake, Meneja wa TFDA wa Kanda ya Mashariki, Emmanuel Alfonce amesema uchunguzi wa awali walioufanya kwenye lebo ya mifuko hiyo unaonyesha uliwekwa Oktoba, 2015 na matumizi yake yanamalizika Oktoba 2017.

Alfonce amesema kwamba, taarifa zilizagaa kutoka eneo la Feri-Kigamboni kuwa kuna mchele unaotoa harufu ambao unauzwa na kwamba, watu wanaofia kuutumia kwa chakula.

Mapema mwaka jana, hofu iliibuka ya kuwapo kwa mchele wa plastiki jambo ambalo lilipingwa na TFDA.
Mpya zaidi Nzee zaidi